Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Iran,Urusi na Uturuki zimejiweka pamoja kuunda nguvu ya muungano wa mataifa matatu wenye lengo la kuimarisha hatua kujiingiza Syria, na kuchukua fursa ya kusitasita mataifa ya magharibi kujiingiza kijeshi nchini humo.
Marais wa mataifa hayo matatu , Vladimir Putin , Recep Tayyip Erdogan , na Hassan Rouhani wa Iran , ambao kwa muda mrefu walionekana kuwa mahasimu wa kimkoa badala ya washirika wa kimkakati, watakutana leo mjini Ankara kwa mkutano wao wa pili wa kilele kuhusu Syria katika hatua ya kuonesha umoja wao.Mkutano huu , ambao unafuatia mkutano wa kwanza wa kilele baina ya viongozi hao mjini Sochi Novemba mwaka jana, unakuja wakati Uturuki ikiwania kupata sauti kubwa baada ya kuazisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi ndani ya Syria.
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba nchi yake itakuwa inajiondoa "hivi karibuni" kutoka Syria , katika hatua ambayo itaimarisha ushawishi wa Uturuki , Urusi na Iran nchi ambazo zimekuwa na majeshi yao ndani ya nchi hiyo.
Sinan Ulgen , mwenyekiti wa kituo cha sera za mchanganuo wa mawazo katika masuala ya kiuchumi na sera za mambo ya kigeni cha mjini Istanbul, amesema mataifa hayo matatu sasa yamekuwa wadhibiti wakuu ndani ya Syria.
Ulgen aliongea na waandishi wa habari kwamba mataifa hayo matatu yamekuwa "mataifa yenye nguvu kimkoa ambayo yako tayari kuwekeza rasilmali za kijeshi kushawishi matokeo ya mzozo huo."
Mataifa hayo matatu mwaka jana yalianzisha mchakato wa kuleta amani sambamba na mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa mataifa mjini Geneva. Mazungumzo hayo , ambayo yanafanyika Astana, yamefanyika mara kadhaa bila ya kupata suluhisho.
Uturuki ambapo nyuma yake kuna mataifa ya kiarabu na mataifa ya kimagharibi wanadhamini upande wa magaidi na wapinzani huku Iran na Urusi zikiisaidia serikali kupambana na makundi hayo.
Mchakato wa wa amani wa Astana
"Mchakato wa mjini Astana ni chombo ambacho Uturuki , Urusi na Iran , vinakiangalia kuweza kudhibiti vita na kupata maslahi yao mbali mbali," amesema Elizabeth Teoman , mchambuzi wa Uturuki katika taasisi iliyoko mjini Washington katika mitaala ya vita (ISW).
Urusi ina uwezo mkubwa wa nguvu za angani nchini Syria wakati Iran inadhibiti nguvu za jeshi la ardhini ,Lakini Erdogan ameongeza ushawishi wa Uturuki kwa kuazisha mwezi Januari mashambulizi kuukamata ardhi kutoka kwa vikosi vya wanamgambo wa ulinzi wa umma vya Wakurdi vya YPG.
Mashambulizi hayo tayari yamefanikisha kukamatwa kwa eneo la zamani wa YPG la Afrin na Erdogan ametishia mara kadhaa kuendeleza msukumo wake kuelekea zaidi upande wa mashariki.
"Erdogan ni mshirika dhaifu kwa misingi wa majeshi ya ardhini na udhibiti wa anga. Lakini amejenga uwiano na kuthibitisha kwamba anaweza kujenga uwezekano ndani ya nchi hiyo," amesema Teoman.
Lakini wachambuzi bado wana shaka juu ya uwezekano wa muda mrefu wa utendaji wa muungano huo kati ya mataifa hayo makubwa matatu ambayo yametumia historia yao kubwa ya vita na kupigana vikumbo kuwania ushawishi katika eneo hilo la bahari nyeusi. Kinadharia bado wanaendelea kuwa katika pande zinazotofautiana katika mzozo huo , ambapo Urusi na Iran zikitoa usaidizi wa kijeshi kwa utawala wa Syria wa rais Bashar al-Assad lakini Uturuki na wenzake wa Magharibi wanaunga mkono wapinzani na magaidi.
Mwisho wa habari/ 291